Michezo

Michezo katika eneo la kilimanjaro.

Michezo hasa hasa mpira wa miguu unahamasisha watu wa Tanzania pia.Karibia kila kijiji na shule unakuta eneo la kucheza mpra. Lakini pia wanapenda kucheza mpira wa kikapu na netball sana.

Hali ya viwanja vya michezo na vifaa sio nzuri na pia kuna waalimu wachache waliofudhu kwenye kufundisha michezo.Na hakuna mpangilio mzuri wa ratiba za michuano.sana sana kwenye maeneo ya vijijini.Kwa miaka mingi RAFIKI ev.imesaidia kuwepo kwa michezo mashuleni na pia nje ya shule.

Miradi bora ambayo ilianzishwa ni mpira wa miguu kwa wasichana na rugby ambayo imekuwa ikiendelea kukuzwa,sio tuu na vijana wetu wanaofanya kazi ya kujitolea kutoka Ujerumani tuu ila shukrani kwa mfanyakazi mwenzetu kutoka Tanzania Rehema Mselle anayefanya kazi kwa bidii.Ushirikiano huu umeonekana katika mechi ya wanafunzi wasichana wa KIUMAKO na KIUMO dhidi y atimu ya wanawake ya Kellinghusen mwezi julai mwaka 2013 katika uwanja wa shule ya msingi Mwika.

 

Wasichana wakiwa wamevaa kaptula za michezo  na michuano ya RAFIKI.

Oliver Zantow

Katika mwaka 2004 tulitengeneza mafunzo ya walimu wa KIUMO asubuhi . na mchana tukapendekeza kucheza.kugawanya makundi tuliuliza nani anapenda kucheza mpira wa wavu?:wasichana wote wakanyanyua mikono juu.na nani atapenda kucheza mpira wa miguu:wavulana wote wakasema watacheza.

Tukawauliza wasichana kama wachache wao watapenda kucheza mpira wa miguu.:wakashangaa na kukaa kimya.basi,”atakayetaka kuja kucheza mpira wa miguu kama kutakuwa na wasichana tutakuwa tunacheza kwa kubadilishana siku moja na wavulana na siku nyingine na wasichana”

La hasha!kwa ule muda kulikuwa na wasichana waliovutiwa kucheza mpira wa miguu.tulicheza nao mpira wa miguu kawaida kwenye mechi ya kuhitimisha.Hii ilisababisha kujaa kwa kelele kutoka kwa wavulana waliojificha na maneno ya kijinga.kwa sababu eneo la mpira wa miguu  sio kwa wasichana. Hata kama wakiwa wamevaa sketi juu ya kaptula zao za kuchezea. Karibia wote walikuwa wanacheza peku na wengine na malapa kwa sanbabu kwa wasichana sio wote walikuwa na viatu vya shule kwahiyo inakuwa ngumu kwa mwanafunzi kuwa na viatu vya michezo.

Mwisho wa mafunzo yetu kwenye karakana timu mbili ya wavulana zilicheza dhidi ya timu mbili za wasichana.wanafunzi wa mwaka wa kwanza dhidi yam waka wa pili.Mechi ya wasichana ilikuwa tamasha kubwa na watu wengi hawakutaka kukosa hii mechi.

Kimsingi hii ndo ilikuwa ishara ya RAFIKI kutangaza michezo. Wakati mwingine tulipoenda Tanzania tulipeleka jezi za michezo kwa wasichana waliokuwa bado na shauku ya kucheza mpira wa miguu.Tokea siku hiyo  mwalimu wa michezo wa KIUMO James Mmbando anacheza mpira na wanafunzi wavulana na wasichana. Na mara kwa mara kunakuwa na michuano dhidi ya shule nyingine.

Sasa tulitaka kuona wasichana wakucheza wakiwa wamevaa jezi mpya.Baada ya hapo wavulana pia wakataka kucheza kwahiyo zikawa timu mbili za wavulana.

Kwa kawaida giza linaingiaga karibia na saa moja usiku kila siku.Hiyo ilileta ulazima wa ratiba maalumu kutengenezwa .Ambayo ilikuwa ngumu kwa watanzania kwa kuwa swala la muda kwao ni shida.Hata hivyo sababu iliyosababisha watu waliokuwa uwanjani kuendelea kuwa na woga ni kuwa wasichana hawakutoka kwenye chumba chao cha kubadilishia nguo(darasa la shule ya jirani) kwa sababu hawakuthubutu kutoka nje na kaptula fupi.Ila baada ya kuongea nao kirafiki baada nya muda walitoka.Japokuwa makelele uwanjani yalikuwa mengi,mechi iliweza kufanyika.

Tunapeleka vifaa muda baada ya muda toka kipindi hicho na wasichana wanacheza mpira kama wavulana.

Kuimarisha jukumu la wanawake katika jamii na kuboresha fahamu binafsi kwa wanawake kwenye mkoa tutaendelea kusaidia mpira kwa wanawake.

Kwenye mpira wa miguu kwa wanaume ni tofauti:wavulana wanakuwa na hamu ya kucheza mpira pale wanapoona mpira mbele ya miguu yao. Kila kijiji kina timu ya mpira wa miguu.Angalau kuna mashabiki wengi wa mpira wa miguu.Tunasaidia mpira wa miguu kwa marafiki wanaocheza mpira wa miguu katika eneo la Kilimanjaro kwa kulipia gharama za kuendesha michuano.

Uandaaji kwa sasa ni kazi ya mwalimu wa kirimeni, Wilbert Nyela.

Mpira wa miguu uliimarishwa sasa sio tena kama tamasha wakati wasichana wakiwa wanacheza mpira wa miguu. imekuwa kawaida sasa. Tunasaidia kwa klabu za michezo za mara kwa mara katika shule ya KIUMAKO na hii ilikuzwa kwa kutembelewa na timu ya wanawake ya VFL kutoka Kellinghusen.

Tunapanga kukuza utangazaji wa michezo zaidi. Shule nyingi hazina masomo ya michezo kabisa kwa sababu hakuna vifaa maalumu na waalimu hawajui jinsi ya kufundisha michezo na pia sheria zake. Tunataka kuweka tabia ya kupenda  kucheza na tunatumaini michezo ambayo inafahamika inaweza kuimarishwa kwenye eneo lote la Moshi kwa kupitia karakana.

 

 

 

Nyuma