Wanafunzi wa mazoezi nchini Tanzania

Kwa kupitia RAFIKI wanafunzi wa ualimu kutoka chuo cha Kiel wameweza kufanya mazoezi yao nchini Tanzania na kupokea cheti kutoka katika shule ya Albechts-university.

Tunafanya kazi pamoja na AG Didaktik der geographie chini ya uangalizi wa Prof.Wilfried Hoppe na LICAU.

Wanafunzi wote wanaoenda Tanzania kufanya mazoezi yao ya ualimu wanashiriki katika warsha ambayo inafanyika kwa washirika wetu BiBeKu GmbH ili kupewa utangulizi. Baada ya hapo tuna saini mkataba wa kufanya mazoezi hayo na pia kuandaa sehemu ya malazi,chakula  na pia usafiri kutoka na kwenda uwanja wa ndege wa Kilimanjaro.

Gharama za mazoezi hayo ni juu ya mwanafunzi mwenyewe.Pia kuna uwezekano wa kuchangiwa fedha ambayo wanafunzi watatangaziwa wakifika kwenye warsha hiyo.

Kupata viza na pia kibali cha kufanya kazi mwanafunzi anatakiwa kulipa mwenyewe.

Kwa sasa gharama za chakula na malazi ni euro 10 kwa siku ambayo ni sisi tunapokea.

Wanafunzi wengi tayari wamepata mada nzuri kwa shahada zao wakati wa mazoezi nchini Tanzania mfano;mfumo wa shule za nchini Tanzania.

Mawasilianao kwa semina za kujiandaa:

Marcus Wack

Marcus.Wack(at)bibeku.de

 

Mawasiliano kwa mohojiano ya awali.

Oliver Zantow

Oliver.Zantow(at)rbz-wirtschaft-kiel.de

Nyuma

 

 

Kwa ushirikiano na: